HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

12 August 2009

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA HABARI NA MCHEZO JOEL NKAYA BENDERA KATIKA VILABU VYA SIMBA NA YANGA

Haijawahi kutokea kwa waziri anayehusika na michezo nchi hii kutembelea vilabu vikubwa vya soka nchini namaanisha watani wa jadi Simba na Yanga lakni Joel Nkaya Bendera amemaliza kwa kutemblea vilabu hvyo nguli Nchini
Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Joel Nkaya Bendera akiwa katika Mazungumzo na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Hasan Dalali Katika makao makuu ya Klabu ya Simba pale Msimabazi
Waziri bendera anapongea mbele ya Wandishi wa Habari huku akiwapa ukweli viongozi na kuwapa changamoto kufika pale ambapo klabu nyingine za afrika zimefika. Hapa sasa Tupo jangwani huyo anaye kunywa maji ni katibu mkuu wa shilikisho la soka tanzania TFF Fredirick Rameck Mwakarebela pembeni yake ni Lucas kisasa pia ni kiongozi katika klabu ya Yanga. Hapa Mh waziri kafika Jangwani na anakaribishwa na mwenyekiti wa yanga IMANI MADEGA
Hawa ni kati ya washabiki na wanachama wa klabu ya yanga waliofika kumsikliza mh Waziri
Imani madega mwenyekiti wa klabu ya yanga akimuonyesha MH bendera sehemu ya kugeshea magari wachezaji wa yanga
Mwekiti wa yanga akiwa ameshikilia suti yake ambayo inaonekana ni ya bei mbaya hapo alikuwa akimwomba aongee na wanachama wa Mh naibu waziri Bendera
Hapa ndipo alipoanza kuwambia ukweli wa mpira unavyoendeshwa duniani na akawapa na mawazo mapya ilikungalia maendeleo ya klabu
Hapa sasa unaweza kumuona mh Bendera anasaina baadhi ya vyeti vya marefaree kutoka kwa katibu mkuu eugine mwasamaki hayupo pichani na ofisi ni ya kufanyia press confrence katika klabu ya yanga
Hii ni sehemu ya juu ambapo wachezaji watakuwa wakipumzika baada ya mechi kuna vivuli ambavyo huwezi kuviona vipo nyuma yangu
Mwenyekiti wa yanga Imani madega akimwonyesha naibu waziri wa habari michezo na utamadu Joel Bendera moja kati ya ofisi za makatibu muhtasi wa klabu ya yanga.
Naam unaona waziri bado yupo fiti sasa hapa alikuwa kwenye Gym ya klabu ya yanga akijaribu kuonysha uwezo wake katika ziara alaiyoifanya klabu ni hapa leo hii.
Sasa kweli yanga imeamua kwani mpaka Rangi ya shuka ni kijani na manjanoNaibu waziri wa habari utamaduni na michezo Joel Bendera akiwa ameshika kitanda kuangalia wa vitanda hivyo.
Hapa anaonyeswha Bwawa la kuogelea wachezaji nadhani itakuwa ndiyo klabu pekee kwa tanzania kufanya vitu adimu kama hivyo.
Mwisho kabisa akapelekwa kwenye uwanja wa kaunda ambapo ndipo yanga inapotumia wa mazoezi na ndiyo uwanja wake wa nyumbani ukiwa kati ukarabati kwa sasa.
NDUGU ZANGUNI SIMBA NA YANGA HUU NDIO WAKATI KWANI WAZIRI AMEWAPA HESHIMA ITUMIE NI ILITUFIKE MBALI ZAIDI.
TUACHE POLOJA TUTENGENEZE SOKA

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers