HABARI MPENZI MWANAMICHEZO KARIBU KATIKA KURASA HII MAHSUSI KWA HABARI ZA MICHEZO PIA UNAWEZA KUTANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU ZAIDI KWA MUDA MREFU ZAIDI WASILIANA NASI KWA NAMBA +255713 15 33 48

11 March 2013

JE MUNGU ANAMPA UHAI WA DAKIKA TANO Andrés Escobar Saldarriaga UNAFIKILI ANGESEMA NINI KUHUSU KAMARI ZA SOKA ?

Andrés Escobar Saldarriaga (13 March 1967 – 2 July 1994), Jina la utani  " Kijana wa  Kandanda ",ni raia wa Colombia na mchezaji ambaye aliuawa kwa kupigwa Risasi huko  Medellín. na inaaminika aliuawa kwa ajili ya kujifunga mwenyewe katika fainali za kombe la dunia za mwaka 1994 Dhidi ya timu ya soka ya taifa ya Marekani ambao ndio waliokuwa wenyeji wa michuano hiyo  na walikuwa wa kiaandaa kwa mara ya kwanza na ubingwa kutwaliza na Brazil 
 http://media.nj.com/nj_soccer/photo/andres-escobar-colombia-own-goal-reax-world-cup-0a4294d601e06619_large.jpg



 http://norwegianmusings.files.wordpress.com/2011/04/andres-escobar-own-goal.jpg 

Escoabar inawezekana mpaka anakufa alikuwa hajui kuwa ameshika mamilino ya watu kwenye mguuu wake ambapo vijana kadhaa walikuwa wakicheza mchezo wakubahatisha kinyemela mchezo uliokuwa unaendeshwa na wauza madawa ya kulevya nchini humo   .

Andrés Escobar  bado ni alama kubwa ya soka hasa kwa Wananchi na mashabiki wa Colombian, na mpaka leo hii anakumbukwa hasa na mashabiki wa  Atlético Nacional's . Kaka yake , Santiago, anamiliki timu kadhaa . Andrés anajulikana kama  "Life doesn't end here".yaani maisha hayaishiii hapa.

  Kijana huyu amakulia  katika familia ya kati  ambapo baba yake  Dario Escobar, alikuwa akifanya kazi Bank na alipata nafasi ya kukusanya baadhi ya vijana wanaozagaa mtaani na kuunda timu yake kucheza soka .Baada  kifo cha   Escobar , Familia iliaanzisha mradi uitwao Andrés Escobar lengo kuu likiwa ni kuwapa  faida watoto ambao wameshindwa maisha na kuanza kucheza mpira kama ajira kwao  kaka yake  , Santiago, alishinda kombe la  Mustang akiwa na  Atlético Nacional.
aliwahi kusoma katika chuo cha  Calasanz na kuhitimu mafunzo na kuingia katika taasisi ya  Conrado Gonzalez. aliishiriki katika timu za shule na aliweza kuwa mchezaji wa kulipwa ,mpaka anakufa  Escobar alikuwa mahusiano ya na mchumba wake ambaye ni mganga wa meno . Escobar aliuawa mwezi mmoja kabla ya kufunga ndoa.

 http://cdn.worldcupblog.org/www.worldcupblog.org/files/2010/02/escobar.png

Escobar alikuwa mlinzi mahiri Colombia katika michuano ya kombe la dunia miaka ya  1990 na  1994. Huku akivalia jezi namba  2, na alipewa jina la utani la  "El Caballero del Futbol" yaani kijana mtanashati wa soka  ambapo alicheza vilabu .  Atlético Nacional na  Young Boys Bern.ya uswis  alikuwa  akijuliakana kwa mabao yake maridadi ya vichwa alianza kucheza soka ya kulipwa mwaka 1988 akiwa na miaka 21  , na aliisaidia Nacional kushinda kikombe cha  Copa Libertadores mwaka  1989.



 http://media3.washingtonpost.com/wp-srv/photo/gallery/100702/GAL-10Jul02-5055/media/PHO-10Jul02-236051.jpg

Lakini ukimtazama Escobar wakati mpira unaingia wavuni katika marejeano ya picha za runinga ni dhahiri anasikitika kwa timu yake kuyaaga mashindano bila kujua kuwa nyumbani kumechezwa kamari ya kubahatisha nani mshindi? na magenge ya wahuni ambao hivi karibuni hata uefa shirikisho la soka la ulaya lilikili kuwa kuwa kuna baadhidi ya mechi zilikuwa zinahushwa na upangaji wa matokeo zipo kamari ambazo zinachezwa ndani sheria na zisizochezwa ndani ya sheria lakini hizi za kiholela ndizo mbaya mbaya zaidi kwani mchezaji anaweza kuwa matatani au viongozi wa timu kwani watu wengi uamua kuchukua sheria mkononi pasipo kufikili kama timu zimefanya makusudi au la .

http://news.bbc.co.uk/olmedia/1630000/images/_1632224_escobar150.jpg

Mambo ya upangaji wa matokeo yanaweza kuonekana ni jambo la kawaida kwa baadhi ya sehemu lakini husababisha matatizo kwa pande mbili aidha timu na wachezaji kufahamu wanachokifanya kuhusu kamari au wasiwe na wanajua lolote kuhusu nini kinaendelea nje ya kiwanja au makasino lakini yote haya huja baada ya tatizo kutokea labda tujiuliza Kwa dakika tano Mungu angemrejesha Duniani Escobar unafikili angesamaje kuhusu kamari za soka . 



 http://ww1.hdnux.com/photos/10/64/43/2312428/7/628x471.jpg
 Nafikili ifike wakati kiundwe chombo aminifu cha kuchunguza matukio ya soka hasa katika matokeo ya mechi kubwa duniani kwani zipo baadhi ya Timu  hufungwa magoli ya kushangaza pasipo kutegemea .

No comments:

Post a Comment

lisungu_chisara@yahoo.com

TUTUMIE HABARI YOYOTE YA MICHEZO, BURUDANI TUTAZICHAPISHA

TANGAZA KWA MFUMO HUU


MAHUDHURIO YA WASOMAJI KIMATAIFA

free counters

Followers